Saturday, March 22, 2014

MAJERUHI YAMKOSESHA VAN PERSIE DERBY SAMBAMBA NA BAYERN.

MSHAMBULIAJI nyota wa Manchester United, Robin van Persie anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kati ya wiki nne mpaka sita kutokana na majeruhi ya mguu aliyopata. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 30 alitolewa nje na machela baada ya kufunga mabao matatu-hat trick katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Olympiakos Jumatano iliyopita. Meneja wa United David Moyes amesema vipimo vya kwanza havikuonyesha ukubwa wa tatizo lakini baada ya kurudiwa tena inaonekana kuwa nyota huyo aliumia kuliko ilivyodhaniwa mara kwanza. Van Persie sasa anatarajiwa kukosa mechi zote za robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.

No comments:

Post a Comment