KLABU ya Zenit St Petersburg imemtangaza rasmi Andre Villas-Boas kuwa meneja mpya wa klabu hiyo ikiwa ni miezi mitatu imepita toka atimuliwe na Tottenham Hotspurs. Kocha huyo wa zamani wa Spurs na Chelsea ambaye ana umri wa miaka 36 amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo ya Urusi ambayo imeng’olewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya na Borussia Dortmund jana usiku. Villas-Boas aliwasili Stamford Bridge akitokea FC Porto mwaka 2011 huku akiwa na mategemeo makubwa lakini alitimuliwa na Chelsea Machi 2012 na baadae kwenda Spurs ambapo napo alitimuliwa Desemba mwaka jana. Akihojiwa Villas-Boas amesema ulikuwa ni uamuzi rahisi wa kujiunga na Zenit na changamoto kubwa aliyokuwa nayo hivi sasa ni kuhakikisha klabu hiyo inacheza kwa umoja ili waweze kupata matokeo mazuri. Kocha huyo amesema malengo yake ni kuipeleka kileleni klabu hiyo na kama wakiweza kushinda mechi tisa zilizosalia katika Ligi Kuu ya Urusi hakuna shaka kwamba watatawazwa mabingwa.
No comments:
Post a Comment