OFISA upelelezi wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA anatarajia kuwahoji wajumbe 12 waliobakia wa kamati ya utendaji ya shirikisho hilo ambao walihusika katika kutoa uamuzi wa kuwapa uenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2022 nchi za Urusi na Qatar. Ofisa huyo Michael Garcia anafuatilia madai kuwa mchakato huo ulifanyika kwa udanganyifu. Kamati ya Utendaji ya FIFA inatarajiwa kukutana jijini Zurich, Uswis kwa ajili ya mkutano wa siku mbili. Rais wa FIFA Sepp Blatter na rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA Michel Platini ni miongoni mwa wajumbe ambao watahojiwa na Garcia. Baadhi ya wajumbe waliohusika katika upigaji kura katika uteuzi huo uliofanyika mwaka 2010, wamestaafu wakati wengine wamefungiwa au kulazimika kujiuzulu baada ya kukutwa na hatia ya taraibu mpya za maadili za FIFA.
No comments:
Post a Comment