Friday, April 4, 2014

BARCELONA WALALAMIKA KUONEWA NA FIFA.

RAIS wa klabu ya Barcelona, Josep Maria Bartomeu amesema Shirikisho la Soka Duniani-FIFA halijawatendea haki kuwafungia kusajili. Barcelona hawataruhusiwa kununua wachezaji mpaka majira ya kiangazi mwaka 2015 baada ya FIFA kuwakuta na hatia ya kuvunja sheria za usajili wa wachezaji walio chini ya umri mara kadhaa. Klabu hiyo imedai kuwa itakata rufani kuhisiana na adhabu hiyo waliyopewa. Bartomeu amesema lazima wapiganie haki yao kwasababu wanadhani adhabu adhabu waliyopewa haikuwastahili.

No comments:

Post a Comment