Friday, April 4, 2014

SUNDERLAND YALIMWA FAINI KWA KUMCHEZESHA MCHEZAJI ASIYERUHUSIWA.

KLABU ya Sunderland imelimwa faini na Ligi Kuu nchini Uingereza baada ya kumchezesha mchezaji asiyeruhusiwa katika mechi nne za ligi mapema msimu huu. Mshambuliaji Ji Dong-Won mwenye umri wa miaka 22 alicheza katika mechi dhidi ya Fulham, Southampton, Crystal Palace na Manchester United kabla ya Sunderland hawajaarifu uongozi wa Ligi Kuu kufanya makosaa ya kiutawala. Sunderland wamelimwa faini hiyo kwasababu ya kushindwa kupata vibali vya kimataifa kwa ajili ya mchezaji huyo raia wa Korea Kusini baada ya kurejea klabuni hapo kutoka timu ya Augsburg ya Ujerumani alikokwenda kwa mkopo msimu uliopita. Klabu hiyo haitakatwa alama kwa mechi zote walizomchezesha nyota huyo.

No comments:

Post a Comment