Friday, April 4, 2014

BENTEKE KUKOSA KOMBE LA DUNIA.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Aston Villa, Christian Benteke atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi kisichopungua miezi sita baada ya kuumia msuli. Nyota wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 23 anatarajiwa kufanyiwa upasuaji baada ya kupata majeruhi hayo wakati mazoezi ambapo itamfanya pia kukosa michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika baadae mwaka huu. Meneja wa Villa Paul Lambert amesema ni pigo kubwa kwa klabu na mchezaji mwenyewe lakini anaamini atafanya bidii kwasababu ndivyo anavyofanya na atarejea tena uwanja akiwa fiti zaidi msimu ujao. Benteke ambaye alinunuliwa kwa paundi milioni saba kutoka katika klabu ya Genk ya Ubelgiji amefunga mabao 23 katika mshindano yote msimu huu na alikuwa akihusishwa na tetesi na kuondoka Villa Park.

No comments:

Post a Comment