MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Manchester United, Javier Hernandez ameambiwa kuwa timu hiyo iko tayari kumuuza katika majira ya kiangazi baada ya kulalamika kunyimwa nafasi ya kucheza mara kwa mara. Hernandez amezungumza na meneja wa United David Moyes karibu mara tatu kwenye miezi miwili iliyopita juu ya kutofurahishwa kwake kwa kukosa nafasi ya kucheza akiwa amepangwa mara tano pekee katika kikosi cha kwanza msimu huu. Nyota huyo wa kimataifa wa Mexico ameiambia United kuwa atasikiliza ofa zitakazokuja kwa ajili yake katika majira ya kiangazi kwakuwa anadhani hayupo katika mipango ya Moyes ambaye ameonekana kuwapa nafasi sana Wayne Rooney, Robin van Persie na Danny Welbeck. Kutokana na hilo Hernandez amekuwa akitaka kuondoka na amekuwa akihusishwa na kuhamia Atletico Madrid kuchukua nafasi ya Diego Costa ambaye anakaribia kutua Chelsea. United imepanga kuimarisha chake katika majira ya kiangazi na tayari nahodha wake Nemanja Vidic akiwa tayari amesajiliwa na Inter Milan wakati Rio Ferdinand, Patrice Evra, Shinji Kagawa, Nani, Anderson na Alex Buttner wakiwa mojawapo ya wachezaji wanategemewa pia kuondoka kiangazi.
No comments:
Post a Comment