Sunday, April 20, 2014

FALCAO ANAWEZA KWENDA BRAZIL - DAKTARI.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao kuna hati hati ya kutokuwa fiti mwanzoni mwa michuano ya Kombe la Dunia kwa mujibu wa daktari aliyemfanyia upasuaji lakini anaweza kuwemo katika kikosi cha nchi hiyo. Falcao mwenye umri wa miaka 28 akuwa nje ya uwanja toka alipoumia vibaya goti lake katika mchezo wa Kombe la Ufaransa dhidi ya Chasselay Januari mwaka huu. Nyota huyo ambaye amefunga mabao tisa katika mechi 17 alizocheza msimu huu, hivi sasa anakimbizana na muda katika mazoezi yake ili aweze kuchaguliwa kwa ajili ya Kombe la Dunia. Daktari wake Jose Carlos Noronha anategemea falcao kuwemo katika kikosi cha nchi hiyo kitakachokwenda katika michuano hiyo nchini Brazil hata kama atakuwa hajapona moja kwa moja. Noronha amesema hadhani kama Falcao anaweza fiti kwa asilimia 100 katika mechi za mwanzoni lakini anaweza kwenda katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment