Sunday, April 20, 2014

MOURINHO ASHANGAZA KWA KUMSIFIA MWAMUZI BAADA YA KIPIGO KUTOKA KWA SUNDERLAND.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho jana alikataa kujibu maswali baada ya kikosi chake kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Sunderland, badala yake alitumia muda huo kumpongeza mwamuzi Mike Dean pamoja na bosi wao Mike Riley. Dean aliizawadia penati Sunderland ambayo iliamua mchezo huo na kuiacha Chelsea ikififisha matumaini yao ya kunyakuwa taji la Ligi Kuu kwa kuwa nyuma ya Liverpool kwa alama mbili huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi. Katika hali ya kushangaza katika mkutano na waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo, Mourinho alimsifia mwamuzi huyo kwa kuchezesha vizuri ingawa timu yake ilipoteza mchezo. Mbali na kumsifu mwamuzi huyo lakini aliendelea kwa kumsifia ofisa mkuu wa Cham Cha Waamuzi nchini humo Mike Riley kwa kazi nzuri aliyofanya katika msimu wote. Mourinho amesema Dean alichezesha vizuri na wakati waamuzi wanapochezesha vyema ni sawa kama ukiwapongeza.

No comments:

Post a Comment