RAIS wa klabu ya Barcelona, Josep Maria Bartomeu ameondoa uwezekano wa kumuuza Lionel Messi na kubainisha kuwa klabu hiyo imepanga kuboresha zaidi mkataba wake. Kumekuwa na taarifa kuwa Barcelona inajipanga kuuza rasilimali yao ghali zaidi kwa ajili ya kujenga upya kikosi cha timu hiyo kufuatia kung’olewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kuteleza mpaka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa La Liga na kufungwa na Real Madrid katika fainali ya Kombe la Mfalme. Hata hivyo, Bartomeu alikanusha taarifa hizo na kuwahakikishia mashabiki wa Barcelona kuwa klabu hiyo haina mpango wa kumuuza Messi na kufafanua kuwa badala yake wanajipanga kumpa mkataba mnono zaidi. Bartomeu amesema wanachotaka kufanya wao ni kuboresha mkataba wake ili uendane na hali ya soka ya sasa ili aweze kuendelea kufanya aliyokuwa akiyafanya mpaka sasa.
No comments:
Post a Comment