Thursday, April 17, 2014

KAMA ULI-MISS VITU ADIMU VYA BALE KATIKA EL CLASSICO JANA.



KIUNGO mahiri wa klabu ya Barcelona, Xavi amekiri kuwa walishindwa kukabiliana na mashambulizi ya ghafla kutoka kwa wapinzani wao Real Madrid hatua ambayo ilipelekea kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali wa Kombe la Mfalme uliochezwa jana usiku. Alikuwa ni Angel Di Maria aliyewapa Madrid bao la kuongoza kabla ya Marc Bartra hajaisawazishiwa Barcelona katika kipindi cha pili, lakini Gareth Bale ndio alikuwa shujaa wa mchezo huo kwa kuifungia bao la ushindi Madrid katika dakika za majeruhi na kuwawezesha kunyakuwa taji hilo. Akihojiwa na mtandao wa klabu hiyo Xavi amesema Madrid walitumia vyema silaha walizonazo kwa kutumia udhaifu wao wa kushindwa kukabiliana na mashambulizi ya ghafla, na anawapongeza kwa hilo. Kiungo huyo amesema walitamani kushinda taji hilo kwa ajili ya mashabiki wao ingawa imeshindikana ila wana nafasi ya kunyakuwa taji la La Liga ingawa amekiri itakuwa kazi ngumu. Barcelona wataingia katika Uwanja wa Camp Nou kukabiliana na Athletico Bilbao katika mchezo wa La Liga utakaochezwa Jumapili.

No comments:

Post a Comment