KLABU ya Chelsea iko mbioni kutumia kitita cha euro milioni 42.5 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji nyota wa Atletico Madrid Diego Costa. Wawakilishi wa Chelsea tayari wameshafanya mikutano kadhaa na kambi ya Costa mwezi uliopita na mazungumzo zaidi yamepangwa kufanyika katika nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya timu hizo. Inaonekana kuwa katika mazungumzo yao Chelsea wako tayari kulipa kitita cha euro milioni 42.5, ingawa kiwango hicho kinajumuisha ada ya uhamisho pamoja na wakala. Chelsea ambao ni mabingwa wa michuano ya Europa League msimu uliopita pia wanaandaa zaidi ya mara tatu ya mshahara wa sasa wa Costa ambapo anakadiriwa kupata kiasi cha euro 61,000 kwa wiki akiwa Atletico. Kocha wa Atletico tayari ameshatoa baraka zake kwa nyota huyo kuondoka kwa kukiri kuwa klabu hiyo haina uwezo wa kumzuia asiuzwe kwenda timu zenye nguvu ya kifedha.
No comments:
Post a Comment