Thursday, April 17, 2014

MOYES NDANI YA JIJI LISBON KUWAFUATILIA KINA MANGALA.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, David Moyes alisafiri kwenda jijini Lisbon jana kufuatilia mchezo uliowakutanisha timu mahasimu kati ya Benfica na FC Porto. Madhumuni ya kuhudhuria mechi hiyo ya nusu fainali ya Kombe la Ureno yalikuwa mahsusi kwa ajili ya kuwafuatilia baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa wakifuatiliwa na wang’amuzi wa vipaji wa United. Mfungaji anayeoongoza wa Porto Jackson Martinez, beki wa kati wa kimataifa wa Ufaransa Eliquiam Mangala na beki wa Benfica Ezequiel Garay wote wapo katika orodha ya United ya wachezaji ambao wanaweza kusajiliwa ili kuimarisha kikosi cha timu hiyo. Wachezaji wote hao watatu walikuwa katika vikosi cya timu zao kwenye mchezo huo ambao Benfica walishinda kwa mabao 3-1 wakati Moyes akiangalia kutoka jukwaani kwenye Uwanja wa Da Luz. Moyes amekuwa akilalamikiwa mara kwa mara kwa kiwango kibovu kilichoonyeshwa na United katika kampeni zake za kwanza msimu huu akitumia wachezaji aliwarithi kutoka kwa Sir Alex Ferguson. Hata hivyo ingawa kibarua chake hakina uhakika wa kutosha, ameruhusiwa kuendelea na mipango ya kuimarisha kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.

No comments:

Post a Comment