KOCHA wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps haamini kuwa timu kama timu yake inapewa nafasi ya kunyakuwa Kombe la Dunia linatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni mwaka huu. Ufaransa iling’olewa katika hatua ya makundi katika michuano hiyo mwaka 2010 huku wakifuzu kwenda Brazil baada ya kuifunga Ukraine katika mechi ya mtoano na Deschamps anafikiri timu hiyo sio tishio tena kama zilivyo timu zingine hivi sasa. Deschamps amesema kuna timu sita au saba ambazo zinakwenda katika michuano hiyo kushinda lakini Ufaransa haiku katika orodha hiyo. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa madhumun yao ni kushinda mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Honduras utakaochezwa Juni 15 na baadae kuendelea kushinda kufanya hivyo kwa kila mchezo utakaofuata.
No comments:
Post a Comment