Wednesday, April 16, 2014

TAJIRI WA PSG AMKINGIA KIFUA BLANC.

RAIS wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG, Nasser al-Khelaifi amepuuza tetesi zilizozagaa kuhusu mustakabali wa kocha wake Laurent Blanc kwa kuahidi kumuunga mkono. Blanc amekuwa akishambuliwa kufuatia PSG kung’olewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Chelsea baada ya kushindwa kuulinda ushindi wao wa mabao 3-1 na baadae kupoteza mchezo dhidi ya Olimpique Lyon kwa kufungwa bao 1-0. Pamoja na hayo Al-Khelaifi amemtetea kocha huyo kwa kumuahidi kuwa kibarua chake kiko salama na angependa kumuana anaendelea kuinoa timu hiyo katika siku nyingi zijazo. Bilionea huyo kutoka Qatar aliendelea kudai kuwa matokeo yoyote ya uwanjani hayawezi kubadilisha nia yake ya kumtaka kocha huyo kubakia. PSG ina nafasi ya kulipiza kisasi kwa Lyon wakati watakapokwaana kwenye fanali ya Kombe la Ligi Jumamosi hii.

No comments:

Post a Comment