Wednesday, April 16, 2014

GUARDIOLA AIGWAYA MADRID.

MENEJA wa klabu ya Bayern Munich Pep Guardiola anaamini kuwa hawatakuwa na nafasi mbele ya Real Madrid katika mchezo wao wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kama hawatakuwa katika kiwango chao cha juu. Bayern wamekuwa wakihangaika kurejea katika kiwango chao katika siku za karibuni ambapo wamefanikiwa kushinda mechi moja pekee kati ya tano walizocheza hivyo kumchanganya Guardiola. Akizungumza na vyombo vya habari Guardiola amesema kama wakicheza na Madrid kama walivyocheza katika mechi za karibuni hawatakuwa na nafasi ya kufika fainali. Kocha huyo ametoa hali ya tahadhari kuwa wako katika hali ya hatari na wanachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wanarejea katika kiwango chao kabla ya kuivaa Madrid wiki ijayo. Mchezo wa mkondo wa kwanza baina ya timu hizo kwenye nusu fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu April 22 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment