Wednesday, April 16, 2014

CAMPBELL AAHIRISHA PAMBANO LAKE ILI AMUUGUZE BABA YAKE.

MSHINDI wa medali ya dhahabu katika michuano ya olimpiki kwa upande wa masumbwi, Luke Campbell ameamua kupumzika mchezo huo baada ya baba yake kugundulika kuwa na saratani. Bondia huyo mwenye umri wa miaka 26 wa uzito wa banta ambaye ameshinda mapambano yake yote matano aliyocheza toka aanze kucheza ngumi za kulipwa alikuwa na pambano alilotakiwa kucheza Jumamosi jijini Manchester. Lakini alilazimika kuahirisha pambano hilo ili aweze kuwa karibu na familia yake kwa ajili ya kumuuguza baba yake. Akihojiwa Campbell amesema miezi michache iliyopita imekuwa migumu sana kwa familia yake na amekuwa akipata wakati mgumu pia katika mazoezi yake ndio maana ameamua kutopigana kwenye pambano hilo. Campbell alimchapa John Joe Nevin na kunyakuwa medali ya dhahabu katika michuano ya olimpiki mwaka 2012 jijini London.

No comments:

Post a Comment