WAKALA wa Toni Kroos amesisitiza kuwa kiungo huyo wa Bayern Munich hajapokea ofa yoyote kutoka klabu ya Manchester United. United imekuwa ikimhusudu nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani na wana ametegemeo ya kumsajili katika majira ya kiangazi kutokana na mazungumzo ya uwezekano wa kumng’oa Bayern kuanza wakati mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya timu hizo. Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa United imeahidi kumpatia Kroos mshahara wa euro milioni 16 kwa mwaka lakini wakala wake Volcker Struth ameweka wazi kuwa hakuna ofa rasmi yoyote iliyotolewa mpaka sasa. Struth amesema vilabu vinavyomtamani nyota huyo havina haja ya kuweka ofa zao mezani kwasababu Kroos ataendelea kubakia Bayern mpaka 2015.
No comments:
Post a Comment