BEKI mahiri wa klabu ya Arsenal, Thomas Vermaelen amesema kila mchezaji wa timu hiyo anataka Arsene Wenger kusaini mkataba mpya na kubakia katika Uwanja wa Emirates. Kocha huyo raia wa Ufaransa tayari ameeleza nia yake ya kubakia lakini bado hajawa tayari kusaini mkataba mpya na kudai kuwa atafikiria kuhusu mstakabali wake mwishoni mwa msimu huu. Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anategemea Wenger ataongeza muda wake wa kubakia katika klabu hiyo yenye London ya Kaskazini ambapo tayari anakaribia kutimiza miaka 18. Vermaelen amesema kila mtu anataka katika klabu hiyo anataka Wenger kubakia kwa muda mrefu zaidi atakavyoweza kwasababu ameifanya mengi mazuri kwa wachezaji na klabu kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment