BINGWA mara nne wa michuano ya Masters, Tiger Woods anatarajiwa kuikosa michuano hiyo baada ya kufanyiwa upasuaji kufuatia maumivu ya mgongo yaliyokuwa yakimsumbua. Woods ambaye anaongoza katika orodha za ubora wa mchezo huo alikosa michuano ya Arnold Palmer ambayo huwa anaitumia kwa ajili ya kujiweka fiti na michuano hiyo mikubwa. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 38 amesema ni jambo lililomhuzunisha lakini hana jinsi inabidi afuate ushauri wa madaktari ili aweze kupona vyema kwa kipindi kirefu kijacho. Woods ambaye hajawahi kukosa michuano ya Masters kwa kipindi cha miaka 19 iliyopita amewahi kushinda mataji manne ambapo mshindi huvalishwa koti la kijani mwaka 1997, 2001, 2002 na 2005.
No comments:
Post a Comment