MENEJA wa klabu ya Manchester United, David Moyes amesema hatarajii kama suala la usajili linaweza kuathiriwa na kushindwa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya mwakani. United ambao wanashikilia taji la Ligi Kuu jana usiku walifungwa na Bayern Munich kwa mabao 3-1 hivyo kuondoshwa katika michuano hiyo kwa jumla ya mabao 4-2. Kwa maana hiyo United ambao wanashika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi wako katika hati hati ya kushiriki michuano yoyote ya Ulaya msimu ujao. Moyes amesema wachezaji wote ambao wanataka kuja Old Trafford wanajua kuwa kukosekana katika michuano hiyo sio suala la kudumu kwa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment