Wednesday, April 9, 2014

WACHEZAJI WALIWANYIMA MUDA WA KUFIKIRI BARCELONA - SIMEONE.



MENEJA wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone amewapongeza wachezaji mbio na jinsi walivyocheza wakati walipoichapa Barceona kwa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hivyo kuvuka na kutinga nusu fainali ya michuano hiyo kwa jumla ya mabao 2-1. Simeone alifurahishwa na juhudi zilizoonyeshwa na wachezaji wake hususani mshambuliaji wake Adrian Lopez ambaye alichukua nafasi ya Diego Costa aliyemajeruhi na kudai kuwa hawakuwapa viungo mahiri wa Barcelona Xavi au Andres Iniesta muda wa kufikiri. Simeone amesema wamefurahi kuifunga timu bora na sasa wamepata muda wa kupumzika na kufikiria mchezo wao wa La Liga Jumapili. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa waliwaacha Barcelona wamiliki mpira katikati lakini wachezaji walifanya kazi kuhakikisha hawawapi muda viungo wao machachari Xavi na Iniesta kufikiria.

No comments:

Post a Comment