Tuesday, April 15, 2014

MAN CITY YAONGOZA ORODHA YA VILABU VINAVYOLIPA MSHAHARA MNONO.

Mmiliki wa klabu ya Manchester City, Sheikh Mansur.
KLABU ya Manchester City imeendelea kuongoza orodha ya timu za michezo zinazolipa vizuri zaidi wakiwa na wastani wa mshahara kwa mwaka unaofikia paundi milioni 5.3 kwa mwaka sawa na paundi 102,653 kwa wiki. Katika orodha hiyo ya vilabu 20 bora, timu tano za Ligi Kuu nchini Uingereza zimeingia ambapo mbali ya City, wapo majirani zao Manchester United wanaoshika nafasi ya nane kwa wastani wa milioni 4.3 wakifuatiwa na Chelsea na Arsenal wanaoongozana katika nafasi ya 10 na 11 kwa kulipa wastani wa paundi milioni 4 na 3.9 kwa mwaka. Vilabu vikongwe vya baseball vya Marekani New Yankees na Los Angeles Dodgers wanakamata nafasi ya pili na tatu wakifuatiwa na vilabu vya Hispania Real Madrid na Barcelona ambao wanakamilisha tano bora katika orodha hiyo.  Timu zilizokuwepo katika kumi bora ni pamoja na timu ya NBA ya Brooklyn Nets waliopo nafasi ya sita, mabingwa wa Ulaya Bayern Munich katika nafasi ya saba na Cicago Bulls katika nafasi ya tisa, Liverpool wenyewe wanafunga orodha hizo kwa kushika nafasi ya 20.

Orodha Kamili ni kama inavyoonekana katika jedwali.
RANK (LAST YEAR)
TEAM
LEAGUE
AV. ANNUAL PAY (WEEKLY)
1 (1)
Manchester City
Premier League
£5,337,944 (£102,653)
2 (5)
New York Yankees
MLB
£5,286,628 (£101,666) 
3 (2)
Los Angeles Dodgers
MLB
£5,119,701 (£98,456) 
4 (3)
Real Madrid
La Liga
£4,993,393 (£96,027) 
5 (4)
Barcelona
La Liga
£4,901,327 (£94,256)
6 (16)
Brooklyn Nets
NBA
£4,485,019 (£86,250) 
7 (9)
Bayern Munich
Bundesliga
£4,402,905 (£84,671) 
8 (12)
Manchester United
Premier League
£4,322,251 (£83,120)
9 (19)
Chicago Bulls 
NBA
£3,985,706 (£76,648) 
10 (8) 
Chelsea
Premier League 
£3,984,536 (£76,626)
11 (15)
Arsenal
Premier League
£3,901,923 (£75,037) 
12 (20) 
New York Knicks
NBA 
£3,862,191 (£74,273) 
13 (14)
Detroit Tigers
MLB
£3,833,510 (£73,721) 
14 (11)
Philadelphia Phillies 
MLB
£3,811,638 (£73,301) 
15 (22)
Boston Red Sox
MLB 
£3,763,451 (£72,374)
16 (17)
Miami Heat 
NBA 
£3,665,215 (£70,485) 
17 (23)
San Francisco Giants
MLB
£3,613,741 (£69,495)
18 (35)
Juventus 
Serie A
£3,512,696 (£67,552) 
19 (7)
LA Lakers 
NBA 
£3,411,402 (£65,604)
20 (21)
Liverpool 
Premier League 
£3,403,783 (£65,457)

No comments:

Post a Comment