Tuesday, April 15, 2014

RONALDO KUIKOSA BARCELONA KESHO.

KLABU ya Real Madrid, imethibitisha kuwa Cristiano Ronaldo atakosekana katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mfalme dhidi ya Barcelona unaotarajiwa kuchezwa kesho. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno aliumia katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund mapema mwezi huu. Ronaldo tayari ameikosa michezo ya La Liga dhidi ya Real Sociedad na Almeria huku akiwa kama mchezaji wa akiba katika mchezo wa marudiano dhidi ya Dortmund. Meneja wa Madrid Carlo Ancelotti amethibitisha kuwa Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 hatamtumia katika mchezo dhidi ya Barcelona kesho ili aweze kupona vizuri majeraha ya msuli yanayomsumbua.

No comments:

Post a Comment