KOCHA wa zamani wa Barcelona, Radomir Antic anaamini kuwa mshambuliaji nyota wa timu hiyo Lionel Messi hakucheza kwa kiwango chake katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid kwasababu ya kuchezeshwa kama winga. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alishambulia sana kwa kukimbia kilometa 6.8 pekee wakati Barcelona wakienguliwa katika michuano hiyo ya Ulaya na Antic anafananisha tukio hilo na Messi chini ya Gerardo Martino na lile la Rivaldo na Louis van Gaal katika msimu wa 1999-2000. Antic amesema Van Gaal alimlazimisha Rivaldo kucheza wingi ya kushoto bila ridhaa yake pamoja na kuonyesha kuimudu vyema nafasi ya mshambuliaji wa kati na matokeo wawili hao walishindwa kuelewana. Kocha huyo anaamini tatizo hilo ndilo lililomkuta Messi kwani haonyesha kuhangaika sana alipochezeshwa upande kwasababu alitaka kufikisha ujumbe kwake kwamba hakupafurahia. Antic amesema klabu hiyo inakabiliwa na wakati mgumu kuwachezesha nyota wake wote kama Neymar, Messi na Andres Iniesta kwa wakati mmoja.
No comments:
Post a Comment