MAHAKAMA ya Rufani ya Kimataifa imetupilia mbali rufani ya timu ya Red Bull waliyokata kupinga dereva wake Daniel Ricciardo kuenguliwa katika mashindano la langalanga ya Australia Grand Prix. Ricciardo mwenye umri wa miaka 24 ambaye ni raia wa Australia aliondolewa katika nafasi ya tatu Machi mwaka huu kwasababu gari alilokuwa akitumia lilitumia mafuta zaidi inavyoruhusiwa na timu yake ilikataa kupunguza matumizi hayo hata walipotahadharishwa. Shirikisho la Kimataifa la mashindano hayo lilidai kuwa mahakama iliamua kushikilia uamuzi wa kwanza ambao ni kuwaondoa Red Bull walioshika nafasi ya tatu katika mashindano ya Australia. Sheria mpya ya matumizi ya mafuta ya kikomo imezua utata baada ya timu nyingi kulalamika kuwa uamuzi utazamwe upya kutokana na injini mpya za magari hayo wanazotumia msimu huu.
No comments:
Post a Comment