Monday, April 14, 2014

MESSI HANA TATIZO LOLOTE - ZUBIZARRETA.

MKURUGENZI wa michezo wa klabu ya Barcelona, Andoni Zubizarreta amesisitiza kuwa hakuna tatizo kutoka kwa Lionel Messi kufuatia kiwango cha chini alichoonyesha katika mchezo dhidi ya Atletico Madrid na Granada. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina amekuwa akishambuliwa baada ya Barcelona kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya katikati ya wiki iliyopita na tena kushindwa kuonyesha makeke yake katika mchezo dhidi ya Granada ambao walitandikwa bao 1-0. Pamoja na hayo, Zubizarreta amedai kuwa Messi mwenye umri wa miaka 26 anajisikia vyema kuwepo Barcelona na anamtegemea kung’ara katika kiwango chake cha kawaida katika mchezo dhidi ya Real Madrid Jumatano. Zubizarreta amesema anafahamu kuwa Messi hana tatizo lolote na hajawawahi kumtilia shaka hata siku moja ila tatizo ni kwamba watu wamezoea kumuona akifanya maajabu yake na kubadilisha mchezo jambo amekuwa hafanyi katika siku za karibuni. Mkurugenzi huyo anaamini Messi atarejea katika kiwango chake bora kwani kila mchezaji lazima apitie vipind vya mpito kama ilivyo kwake sasa hivi.


No comments:

Post a Comment