MWANARIADHA wa kike ambaye alimaliza mashindano ya marathon yaliyofanyika jijini London mwishoni mwa wiki iliyopita anahofiwa kutoroka ili kukwepa kurudi nyumbani kwao Sierra Leone. Mwanadada huyo Mami Konneh Lahun mwenye umri wa miaka 24 mara ya mwisho alionekana baada ya kumaliza mbio za kilometa 42 jana na alitakiwa kurejea nchini kwake leo. Polisi walilazimika kuanza kumsaka baada ya Lahun kushindwa kurejea katika makazi yake ya muda huko Greenwich jana. Mwanadada huyo ndio mwanariadha mwenye kasi zaidi katika mbio za mita 5,000 na 10,000 nchini Sierra Leaone na mwanamke wa kwanza kuiwakilisha nchi hiyo katika mbio za London marathon. Tabia za wanariadha kujificha baada ya mashindano na baadae kuomba hifadhi ya kisiasa na kuishi kama wakimbizi limekuwa ni jambo la kawaida katika mashindano makubwa. Katika michuano ya olimpiki iliyofanyika jijini London mwaka 2012 wanariadha wengi na makocha walitoroka au wengine kuomba hifadhi za kisiasa kutoka hali machafuko nchini katika nchi wanazotoka.
No comments:
Post a Comment