Monday, April 14, 2014

MWEZI UJAO UTAKUWA WA MAFANIKIO - GERRARD.

KIUNGO mahiri na nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard anaamini kuwa mwezi ujao utakuwa muhimu kwa historia yake ya soka kwani amepania kuisadia timu yake kushinda taji lake la kwanza la Ligi Kuu baada ya kupita kipindi cha miaka 24. Kikosi cha Liverpool kinachonolewa na Brandan Rodgers kilifanikiwa kuwafunga mahasimu katika kinyang’anyiro cha ubingwa Manchester City mwishoni mwa wiki na hivyo kuifanya timu hiyo kucheza mechi 10 bila kupoteza hata moja. Chachu hiyo ya ushindi inamfanya Gerrard kuahdi kuwa atacheza kwa uwezo wake wote katika mechi zao nne zilizobakia msimu huu kuhakikisha anatimiza ndoto zake toka alipojiunga na timu akiwa na miaka saba kwa kunyakuwa taji la ligi. Gerrard amesifu wachezaji wenzake kwa kujitoa kwa kila hali msimu huu na kama wakiendelea kama wanavyocheza hakuna shaka kwamba watafanikiwa kunyakuwa taji la ligi.

No comments:

Post a Comment