Sunday, April 20, 2014

RONALDO AANZA MAZOEZI TAYARI KUIKABILI BAYERN.

KLABU ya Real Madrid imepata ahueni kufuatia nyota wake Cristiano Ronaldo kuanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wao wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich. Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 alikosa mchezo wa fainali ya Kombe la Mfalme dhidi ya Barcelona Jumatano iliyopita kutokana na majeruhi ya goti na alitegemewa pia kuukosa mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Bayern Jumatano. Hata hivyo, sasa inaonekana anaweza kuwepo katika mchezo huo baada ya kuonekana akifanya mazoezi na kikosi cha Madrid leo asubuhi. Meneja wa Madrid, Carlo Ancelotti pia amepata ahueni zaidi baada ya beki Marcelo naye kuanza mazoezi kufuatia kukaa nje kwa muda kutokana na majeruhi.

No comments:

Post a Comment