Sunday, April 20, 2014

HAMILTON AIBUKA KIDEDEA TENA KATIKA MASHINDANO YA GRAND PRIX YA CHINA.

DEREVA nyota wa langalanga kutoka timu ya Marcedes, Lewis Hamilton amefanikiwa kushinda mashindano ya Grand Prix ya China ikiwa ni ushindi wake wa tatu mfululizo kwa mwaka huu. Hamilton raia wa Uingereza hiyo inakuwa mara ya kwanza toka aanze kushiriki mashindano hayo kushinda mara tatu mfululizo. Dereva mwenzake kutoka timu ya Marcedes, Nico Rosberg alikamata nafasi ya pili kwa kumshinda Fernando Alonso wa Ferrari aliyeshika nafasi ya tatu akifuatiwa na Daniel Ricciardo wa Red Bull katika nafasi ya nne. Bingwa wa dunia Senastian Vettel ameendelea kusuasua baada ya kushika nafasi ya tano ikiwa na mara ya pili mfululizo anashindwa na dereva mwenzake Ricciardo.

No comments:

Post a Comment