MENEJA wa klabu ya Sunderland, Gus Poyet amekanusha tetesi kuwa atajiuzulu wadhifa wake huo katika timu hiyo ambayo inapambana kutoshuka daraja. Sunderland ambao wanajulikana kama Paka Weusi kwasasa wanashika mkia katika msimamo wa Ligi Kuu na wanakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Manchester City katika Uwanja wa Etihad leo usiku. Hata hivyo, Poyet mwenye umri wa miaka 46 anaamini kuwa mabadiliko ya kocha sio suluhisho la matatizo ya klabu hiyo kwasasa. Poyet amesema inavyoonekana watu wanamtegemea kuondoka lakini hajui kwanini wanadhani hivyo kwasababu yeye mwenyewe hana mpango huo. Sunderland wanadaiwa alama saba ili waondoke katika msitari wa kushuka daraja, na ingawa wana mechi mbili mkononi wanatakiwa kuanza kupata matokeo mazuri haraka.
No comments:
Post a Comment