KLABU ya Tottenham Hotspurs inategemea kuhamia katika uwanja wake mpya wenye uwezo wa kubeba mashabiki 58,000 ifikapo mwaka 2017. Uwanja huo mpya unatarajiwa kuwa pembeni ya uwanja wao wa sasa wa White Hart Lane ambao unauwezo kuingiza mashabiki 36,000. Klabu hiyo inategemea kutoa zabuni kwa ajili ya ujenzi wake baada mwaka huu huku wakitegemea ufunguzi kuwa katikati ya mwaka 2017. Habari za uwanja mpya zimekuja ikiwa ni siku baada ya Tottenham kutangaza faida ya paundi milioni 1.5 katika mwaka wao wa fedha uliopita.
No comments:
Post a Comment