Wednesday, April 2, 2014

TIMU YA WATOTO WA MITAANI YACHACHAFYA BRAZIL.

TIMU ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania kutoka Kituo cha Mwanza inaendelea vizuri katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa Watoto wa Mitaani yanayoendelea Rio de Janeiro nchini Brazil ambapo katika mchezo wake wa kwanza ilitoka sare ya mabao 2-2 na Burundi. Juzi (Machi 31 mwaka huu), timu hiyo inayoongozwa na mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutoka Mkoa wa Mwanza, John Kadutu ilicheza mechi mbili. Katika mechi ya kwanza iliifunga Argentina mabao 3-0 na baadaye ikailaza Nicaragua mabao 2-0. Michuano hiyo ya siku kumi inashirikisha timu kumi. Mbali ya Tanzania, nyingine ni Argentina, Burundi, India, Kenya, Liberia, Marekani, Mauritius, Misri na Pakistan. Kwa wasichana ni Afrika Kusini, Brazil, El Salvador, Indonesia, Msumbiji, Nicaragua, Philippines, Uingereza na Zimbabwe.

No comments:

Post a Comment