KLABU za Manchester City ya Uingereza na Paris Saint-Germain ya Ufaransa watakabiliwa na adhabu baada ya kukiuka maadili ya sheria ya matumizi ya fedha ya Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA. Mbali na hao vilabu vingine vipatavyo 20 vinaaminika kukutwa na hatia ya kuvunja sheria hiyo. UEFA itatoa ofa maalumu kwa vilabu hivyo vilivyokiuka sheria hiyo kuelekea katika mkutano wao utakaofanyika Alhamisi. Adhabu kubwa ambayo ni timu husika kuenguliwa katika michuano ya Ulaya haitarajiwi kuwepo ingawa pia hawakuweka wazi ni adhabu zipi zitaazotolewa kwa timu hizo.
No comments:
Post a Comment