BODI nzima ya uongozi wa Chama cha Soka nchini Uruguay imelazimika kujiuzulu kufuatia mgogoro juu ya vurugu zinazotokea katika mechi za soka. Bodi hiyo imedai kuchukua uamuzi huo ili kupisha watu wengine wenye mawazo tofauti kuongoza chama hicho. Wiki iliyopita rais Jose Mujica aliondoa ulinzi wa polisi katika viwanja vya timu za Penarol na Nacional, ambazo ndio zenye mashabiki wengi nchini humo kufuatia vurugu zilizozuka baada ya mechi. Jumatano iliyopita mashabiki wa Nacional walipambana na polisi baada ya timu yao kufungwa huku polisi kadhaa wakiumizwa na mashabiki hao katika mji mkuu wa Montevideo. Pamoja na kukosekana kwa usalama kufuatiwa polisi kuondolewa, chama hicho kiliamuru timu kuendelea kucheza mechi zao za ligi kama kawaida ingawa umoja wa wachezaji ulikataa.
No comments:
Post a Comment