Monday, May 12, 2014

15 WAPOTEZA MAISHA KWA KUKANYAGANA UWANJANI HUKO DRC.

WATU 15 wameripotiwa kufa kufuatia vurugu zilizozuka katika mechi ya soka jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Taarifa zimedai kuwa vurugu hizo zilianza baada ya polisi kufyatua mabomu ya machovu uwanjani hapo na kusababisha watu kukanyagana wakati wakijaribu kujinusuru ambapo mbali na vifo lakini pia watu zaidi ya 20 wanadai kuumizwa. Vurugu hizo zilianza kutokana na mashabiki wa timu ya ASV iliyokuwa nyumbani kutofurahishwa na kufungwa kwa bao 1-0 dhidi ya TP Mazembe ya Lubumbashi. Wadau mbalimbali wametoa lawama zao kwa Shirikisho la Soka la nchi hiyo kwa kuruhusu mchezo huo kuchezwa katika uwanja usiofaa hivyo kusababisha msongamano mkubwa kutokana na mashabiki wengi waliohudhuria mchezo huo.

No comments:

Post a Comment