KIUNGO mahiri wa klabu ya Manchester City Samir Nasri hategemei kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa Ufaransa baada ya kudai kuwa atashuhudia michuano ya Kombe la Dunia katika luninga. Nasri amerejea katika kiwango chake msimu huu akiwa na City chini ya meneja Manuel Pellegrini wakati klabu hiyo ikinyakuwa taji lake la pili la ligi katika kipindi cha miaka mitatu. Hata hivyo, Nasri haamini kama atapata simu kutoka kwa kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil pamoja na kuwa nyota wa mchezo wa jana dhidi ya West Ham United katika siku ya mwisho mwa msimu. Nasri amesema kama kuanza katika mechi kwenye klabu kama City na kushinda mataji mawili ya ligi haitatosha kwa Deschamps kumuita itakuwa bahati mbaya na hatalaumu kwa chochote kwani atashuhudia michuano hiyo kwenye luninga. Ufaransa itachuana na timu za Switzerland, Ecuador na Honduras katika kundi E.
No comments:
Post a Comment