BEKI wa klabu ya Chelsea, Ashley Cole ameamua kutustaafu kucheza soka la kimataifa baada ya kuachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachokwenda kucheza Kombe la Dunia. Cole mwenye umri wa miaka 33 ameichezea Uingereza mechi 107 huku akicheza katika fainali tatu za Kombe la Dunia. Beki wa kushoto chipukizi wa Southampton Luke Shaw anajumuishwa katika kikosi hicho kinachonolewa na kocha Roy Hodgson atakayetaja kikosi chake kamili baadae leo. Cole amesema alipata simu kutoka kwa Hodgson na kukubaliana kuwa kikosi cha Uingereza kisheheni wachezaji na anafikiri ni vyema akistaafu majukumu ya kimataifa kwasasa. Naye Hodgson alikaririwa akidai kuwa kumuacha Cole katika kikosi chake ni moja ya maamuzi magumu kufanya katika kazi yake.
No comments:
Post a Comment