Monday, May 12, 2014

WENGER AKANUSHA TETESI ZA KUTIMKIA MONACO.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amepuuza tetesi zinazomhusisha yeye kurejea katika klabu yake ya zamani ya Monaco. Kumekuwa na taarifa nchini Ufaransa zinazodai kuwa Monaco ambao wamekuwa washindi wa pili katika kinyang’anyiro cha Ligi Kuu nchini humo kwamba wanapanga kumchukua Wenger huku kocha Claudio Ranieri akitarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu. Mustakabali wa Wenger umekuwa ukizungukwa na utata kwa wiki kadhaa kutokana nay eye mwenyewe kushindwa kusaini mkataba mpya na Arsenal hatua ambayo imezusha tetesi kuwa anataka kuondoka ingawa amejiweka mbali na taarifa za kwenda Monaco. Akihojiwa mara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Norwich City jana, Wenger amesema anaitakia kila la kheri Monaco lakini hana mpango wa kwenda huko.

No comments:

Post a Comment