Monday, May 12, 2014

KLABU KUBWA INASTAHILI MATAJI MENGI - PELLEGRINI.

KLABU ya Manchester City imepanga kuendeleza utawala wake baada ya kushinda taji la pili la Ligi Kuu katika kipindi cha miaka mitatu. City wanaonolewa na Manuel Pellegrini waliitandika West Ham United na kufanikiwa kushinda taji lao la nne katika ligi katika siku ya mwisho mwa msimu. Akihojiwa Pellegrini amesema timu kubwa haiwezi kuridhika na taji moja, klabu na wachezaji wanastahili mataji zaidi. Pellegrini amesema msimu ulikuwa mzuri kwasababu walikuwa katika mbio za kuwania mataji yote manne kwa kipindi kirefu kuliko timu yoyote Uingereza na wameshinda mawili kati ya hayo hivyo ameridhishwa.

No comments:

Post a Comment