RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter ametoa dokezo lingine kuwa amepanga kutetea kiti chake hicho kwa mara ya tano katika uchaguzi wa shirikisho hilo mwaka ujao. Blatter alikaririwa na gazeti la nchini Uswis akidai kuwa anataka kufanya hivyo kwasababu anaona bado hajamaliza. Gazeti hilo liliendelea kumkariri rais huyo akidai kuwa uongozi wake unafikia kikomo lakini mipango yake aliyoweka bado haijakamilika. Blatter mwenye umri wa miaka 78 alichaguliwa bila kupingwa katika kipindi chake cha nne mwaka 2011 baada ya mpinzani wake Mohamed Bin Hammam kujitoa baada ya kutuhumiwa kutoa rushwa ili aweze kupigiwa kura hatua ambayo ilipelekea kiongozi huyo kufungiwa maisha baadae. Rais huyo aliwahi kusema kwamba kipindi hiki kitakuwa cha mwisho kwake lakini Februari mwaka huu alibadili mawazo hayo na kudai kuwa anajiona yuko katika afya njema hivyo haoni sababu ya kishindwa kufanya kazi na kama akihitajika kugombea hatakataa wito huo.
No comments:
Post a Comment