KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque anatarajia kukosa huduma ya Thiago Alcantara katika michuano ya Kombe la Dunia kiangazi hiki baada ya kiungo huyo wa Bayern Munich kuumia goti. Nyota mwenye umri wa miaka 23 alikuwa ameanza mazoezi ya kawaida baada ya kukaa nje kwa muda kidogo kutokana na majeraha mengine ya goti na alikuwa akitegemewa kurejea uwanjani katika mchezo wa fainali ya DFB Pokal dhidi ya Borussia Dortmund. Hata hivyo, taarifa zilizotoka jana zimedai kuwa Thiago amepata majeruhi mengine na Bayern sasa wamethibitisha kuwa Alcantara amepata majeraha ya msuli wa goti ambayo yatamfanya asiwepo katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil. Ofisa mkuu wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge amefafanua kuwa hilo litakuwa pigo kubwa kwa mchezaji huyo kwani amekuwa akitahidi ili aweze kuiwakilisha nchi yake katika michuano ya Kombe la Dunia na sasa ndoto zake zimezimika. Nyota huyo amekuwa kama na bahati mbaya kwani alikosa pia michuano ya Ulaya mwaka 2012 na ile ya olimpiki mwaka huohuo kutokana na majeruhi.
No comments:
Post a Comment