MWANARIADHA nyota wa Ethiopia, Kenenisa Bekele amefanikiwa kushinda mashindano ya Great Manchester Run na kumzidi mpinzani wake Wilson Kipsang wa Kenya. Bekele anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 5,000 na 10,000 alittumia muda wa dakika 28 na sekunde 23 huku Kipsang ambaye anayeshikilia rekodi ya dunia katika marathon akishika nafasi ya pili kwa kupishana sekunde tano. Bingwa wa dunia na olimpiki katika mbio za mita 10,000 Tirunesh Dibaba naye alipata ushindi kwa upande wa wanawake baada ya kumaliza mbio za kilometa 10 kwa kutumia dakika 31.09. Gemma Steel wa Uingereza alishika nafasi ya pili akipishana kwa zaidi ya dakika moja na Muethiopia Dibaba.
No comments:
Post a Comment