Sunday, May 18, 2014

ZIDANE AMVULIA KOFIA RONALDO.

KOCHA msaidizi wa klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane amemsifu Cristiano Ronaldo kwa kuwa akili za ziada na kudokeza kuwa Mreno huyo atashangaza katika michuano ya Kombe la Dunia kiangazi hiki. Mshambuliaji huyo anatarajiwa kuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Atletico Madrid pamoja na kuachwa katika mchezo dhidi ya Espanyol jana kutokana na wasiwasi wa majeraha ya msuli yanayomsumbua. Zidane alimpongeza nyota huyo na kudai kuwa ana uhakika kwamba atafanya maajabu katika michuano hiyo itakayofanyika Brazil huku Ureno ikikabiliwa na upinzani kutoka kwa Ujerumani katika hatua ya makundi. Zidane aliendelea kudai kuwa anamuona kila siku mazoezini na hana shaka kuwa ataweza kuonyesha uwezo katika michuano hiyo ka alivyofanya katika klabu hiyo msimu huu.

No comments:

Post a Comment