KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amemteua Frank Lampard kuwa nahodha msaidizi katika kikosi cha nchi hiyo kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil. Kiungo huyo wa Chelsea mwenye umri wa miaka 35 ameichezea Uingereza mechi 103 na atakuwa msaidizi wa Steven Gerrard badala ya mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney. Kocha huyo amesema Lampard amekuwa msaidizi wa Gearrard kwenye unahodha kwa muda sasa hivyo anaona ni sahihi akiendelea kushikilia nafasi hiyo kwenye michuano hiyo kwasababu amekuwa kiongozi mzuri. Lampard amewahi kuvaa beji ya unahodha akiwa na UIngereza mara sita.
No comments:
Post a Comment