Tuesday, May 13, 2014

ATOZWA FAINI KWA KUMDHIHAKI MCHEZAJI MWEZAKE AMBAYE NI SHOGA.

TIMU ya Miami Dolphins imemtoza faini Don Jones baada ya kutoa kauli isiyo sahihi katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuhusu Michael Sam kuwa mchezaji wa kwanza wa Ligi ya Mpira wa Miguu nchini Marekani-NFL aliyejitangaza shoga. Sam mwenye umri wa miaka 24 alichaguliwa na timu ya Saint Louis Rams kwa ajili ya msimu ujao wa NFL na muda mfupi baada ya uteuzi huo Jones aliandika katika twitter yake kauli ya kuchukukizwa na hilo. Kutokana na tukio hilo Jones ametozwa faini ambayo haikuwekwa wazi huku akienguliwa katika timu mpaka atapopata darasa la kumuelewesha. Jones mwenye umri wa miaka 23 kupitia tovuti ya timu yake aliomba radhi kwa Sam kwa kauli yake hiyo aliyotoa katika twitter.

No comments:

Post a Comment