KOCHA wa timu ya taifa ya Ghana, Kwesi Appiah ametaja kikosi chake cha awali kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika kiangazi nchini Brazil. Katika kikosi chake kumekuwa hakuna mabadiliko makubwa ambapo Asamoah Gian, Michael Essien na Sulley Muntari wote wameitwa wakati Stephen Adams amekuwa mchezaji pekee anayecheza ligi ya nyumbani kuitwa katika kikosi hicho. Hata hivyo Jeffrey Schlupp Mghana aliyezaliwa Ujerumani anayecheza Leicester City na mshambuliaji David Accam anayecheza Helsingborg wote wamepewa nafasi ya kumshawishi Appiah kabla hajapunguza kikosi chake na kubakiwa na wachezaji 23 baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Uholanzi unaotarajiwa kuchezwa Mei 31. Ghana wamepangwa na Marekani, Ujerumani na Ureno katika kundi lao.
Kikosi Kamili:
Makipa:Adam Kwarasey, Fatau Dauda, Stephen Adams.
Mabeki: Samuel Inkoom, Daniel Opare, Harrison Afful, Jeffrey Schulp, John Boye, Jonathan Mensah, Jerry Akaminko, Rashid Sumaila.
Viungo: Michael Essien, Rabiu Mohammed, Agyemang Badu, Kwadwo Asamoah, Sulley Muntari, Albert Adomah, Wakaso Mubarak, Christian Atsu, David Accam, Andre Ayew, Afriyie Acquah.
Washambuliaji: Asamoah Gyan, Kevin Prince Boateng, Abdul Majeed Waris, Jordan Ayew.

No comments:
Post a Comment