Tuesday, May 13, 2014

BARCELONA YAJIPANGA KUMCHUKUA LUIS ENRIQUE.

KLABU ya Barcelona inajipanga kumchukua kocha wa Celta Vigo Luis Enrique kuja kuinoa timu hiyo msimu ujao. Kocha huyo ambaye amewahi kuwa kocha wa timu B wa Barcelona amekutana na mkurugenzi wa michezo Andoni Zubizarreta wiki iliyopita nyumbani kwake katika mji wa Gava. Kocha wa sasa Gerardo Martino anatarajiwa kuondoka Barcelona kufuatia matatizo mengi ya nje ya uwanja yaliwakumba ikiwemo sakata la uhamisho wa Neymar, kuachia ngazi kwa rais wake Sandro Rosell na kifo cha kushtusha cha kocha wa zamani Tito Vilanova mwezi uliopita. Enrique ilikuwa achukue mikoba ya kuinoa Barcelona wakati Vilanova alipoachia ngazi kutokana na matatizo ya kiafya lakini alikuwa tayari ameshakubali kuifundisha Celta Vigo hivyo Barcelona kuamua kumchukua Martino.

No comments:

Post a Comment