BEKI mahiri wa klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand anatarajiwa kuondoka majira ya kiangazi baada ya kushindw akuongezwa mkataba mpya. Kuondoka kwa beki huyo mwenye umri wa miaka 35 kunamaliza miaka 12 ya utumishi wake hapo ambapo amecheza mechi 454 na kufunga mabao nane. Ferdinand alikaririwa akidai kuwa baada ya kuitumikia timu hiyo kwa kipindi hicho anadhani ni wakati muafaka kwake kuendelea mahala pengine.
Inafahamika kuwa Ferdinand bado anapenda kuendelea kucheza lakini haijulikani na timu gani atakyokwenda.
No comments:
Post a Comment